Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, (tukasema): Enyi milima! Karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia. Na tukamlainishia chuma. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika tulimpa Dāwūd unabii, Kitabu na ujuzi, na tukayaambia majabali na ndege, «Takaseni pamoja naye!» (Dāwūd anapomtakasa Mwenyezi Mungu kwa kuleta tasbihi, fanyeni hivyo pamoja naye). Na tulimlainishia chuma kikawa ni kama unga uliokandwa, anakisinyanga anavyotaka.