Sema: Ikiwa mimi nimepotea, basi nimepotea kwa kudhuru nafsi yangu mwenyewe. Na ikiwa nimeongoka, basi ni kwa sababu ya kunifunulia Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Aliye karibu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, «Nikipotoka nikawa kando na haki, basi dhambi la upotevu wangu liko juu ya nafsi yangu, na nikiwa nitalingana sawa juu ya haki, ni kwa wahyi wa Mwenyezi Mungu Ambao Ananiletea mimi. Hakika Mola wangu ni Msikizi wa ninayowaambia, Yuko karibu na yule anayemlingania na kumuomba.»