Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Saba 34:54

34:54
وحيل بينهم وبين ما يشتهون كما فعل باشياعهم من قبل انهم كانوا في شك مريب ٥٤
وَحِيلَ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ مَا يَشْتَهُونَ كَمَا فُعِلَ بِأَشْيَاعِهِم مِّن قَبْلُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ فِى شَكٍّۢ مُّرِيبٍۭ ٥٤
وَحِيلَ
بَيۡنَهُمۡ
وَبَيۡنَ
مَا
يَشۡتَهُونَ
كَمَا
فُعِلَ
بِأَشۡيَاعِهِم
مِّن
قَبۡلُۚ
إِنَّهُمۡ
كَانُواْ
فِي
شَكّٖ
مُّرِيبِۭ
٥٤
Na watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayo yatamani, kama walivyo fanyiwa wenzao zamani. Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kutawekwa kizuizi baina ya wakanushaji na kile wanachokitamani cha toba na kurudi ulimwenguni wapate kuamini, kama vile Mwenyezi Mungu Alivyowafanya wale wanaofanana na wao miongoni mwa wakanushaji wa watu wa mataifa yaliyopita. Kwa kweli wao walikuwa duniani wako kwenye shaka yenye kutia wasiwasi na babaiko kuhusu jambo la Mitume, kufufuliwa na kuhesabiwa, na kwa hivyo hawakuamini.