Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hiki ulicholetewa kwa njia ya wahyi, ewe Mtume, ni Kitabu tulichokuteremshia kilichobarikiwa, ili wafikirie juu ya aya zake na wazitumie njia zake za uongofu na ishara zake njema, na ili wapate kukumbuka watu wenye akili timamu yale Aliyowalazimisha Mwenyezi Mungu.