Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wakumbuke, ewe Mtume, waja wetu: Ismā'īl, Ilyasa' na Dhulkifl kwa utajo mzuri sana. Na kila mmoja miongoni mwao ni katika watu wema ambao Mwenyezi Mungu Aliwachagua miongoni mwa viumbe na Akawachagulia hali na sifa kamilifu kabisa.