Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu, 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu wako, «Hakika mimi ninawaonya nyinyi na adhabu ya Mwenyezi Mungu isiwashukie kwa sababu ya kumkanusha kwenu Mwenyezi Mungu, hakuna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye Peke Yake, Yeye Ndiye Aliyepwekeka kwa ukubwa Wake, majina Yake, sifa Zake na matendo Yake, Mwenye kutendesha nguvu Anayekilazimisha kila kitu na kukishinda.