Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
038

Sad 38:74 الا ابليس استكبر وكان من الكافرين ٧٤

38:74
إِلَّآ
إِبۡلِيسَ
ٱسۡتَكۡبَرَ
وَكَانَ
مِنَ
ٱلۡكَٰفِرِينَ
٧٤
Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri. 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

isipokuwa Iblisi Yeye hakusujudu kwa ujeuri na kiburi, na alikuwa, katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, ni miongoni mwa makafiri.
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 38, Ukurasa 457, Juzuu 23

71. Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. 72. Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii. 73. Basi Malaika wakat'ii wote pamoja. 74. Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri. 75. Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli? 76. Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. 77. Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika. 78. Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo. 79. Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe. 80. Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula, 81. Mpaka siku ya wakati maalumu. 82. Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote, 83. Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa. 84. kasema: Haki! Na haki ninaisema. 85. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao. 86. Sema (Ewe Mtume) : Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu. 87. Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. 88. Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia