Na hawezi mtu kuamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu iwafike wasio tumia akili zao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Haikuwa nafsi yoyote ni yenye kumuamini Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini Yake na taufiki Yake. Basi usiisumbue nafsi yako katika hilo, kwani mambo yao yako kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Ataajaalia adhabu na hizaya kwa wale ambao hawayatii akilini maamrisho Yake na makatazo Yake.