Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:12

10:12
واذا مس الانسان الضر دعانا لجنبه او قاعدا او قايما فلما كشفنا عنه ضره مر كان لم يدعنا الى ضر مسه كذالك زين للمسرفين ما كانوا يعملون ١٢
وَإِذَا مَسَّ ٱلْإِنسَـٰنَ ٱلضُّرُّ دَعَانَا لِجَنۢبِهِۦٓ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَآئِمًۭا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُۥ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَآ إِلَىٰ ضُرٍّۢ مَّسَّهُۥ ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ١٢
وَإِذَا
مَسَّ
ٱلۡإِنسَٰنَ
ٱلضُّرُّ
دَعَانَا
لِجَنۢبِهِۦٓ
أَوۡ
قَاعِدًا
أَوۡ
قَآئِمٗا
فَلَمَّا
كَشَفۡنَا
عَنۡهُ
ضُرَّهُۥ
مَرَّ
كَأَن
لَّمۡ
يَدۡعُنَآ
إِلَىٰ
ضُرّٖ
مَّسَّهُۥۚ
كَذَٰلِكَ
زُيِّنَ
لِلۡمُسۡرِفِينَ
مَا
كَانُواْ
يَعۡمَلُونَ
١٢
Na mtu akiguswa na shida hutuomba naye kaegesha ubavu, au kakaa, au kasimama. Lakini tukimwondoshea shida yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondoshee shida iliyo mpata. Ndio namna hiyo wamepambiwa warukao mipaka yale waliyo kuwa wakiyatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na impatapo binadamu shida, anatuomba tumsaidiye katika kumuondolea hiyo akiwa katika hali ya kuwa amelala kwa ubavu wake au ameketi au amesimama, kulingana na hali ile alivyo wakati mashaka yalipomshukia. Na tunapomuondolea ile shida iliyompata, huendelea kuifuata ile njia yake ya mwanzo kabla hajapatwa na mashaka na huyasahau yale aliokuwa nayo ya shida na matatizo na huacha kumshukuru Mola Wake aliyemuondolea yale aliyokuwa nayo ya matatizo. Na kama alivyopambiwa binadamu huyu kuendelea katika kukanusha kwake na kuwa na ujeuri baada ya Mwenyezi Mungu kukuondolea mashaka aliyokuwa nayo , vilevile walipambiwa wale waliopita kiasi katika kumzulia Mwenyezi Mungu urongo na Manabii Wake yale ambayo walikuwa wakiyafanya ya kumuasi Mwenyezi Mungu na kumshirikisha.