Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:13

10:13
ولقد اهلكنا القرون من قبلكم لما ظلموا وجاءتهم رسلهم بالبينات وما كانوا ليومنوا كذالك نجزي القوم المجرمين ١٣
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا ٱلْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا۟ ۙ وَجَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ وَمَا كَانُوا۟ لِيُؤْمِنُوا۟ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْقَوْمَ ٱلْمُجْرِمِينَ ١٣
وَلَقَدۡ
أَهۡلَكۡنَا
ٱلۡقُرُونَ
مِن
قَبۡلِكُمۡ
لَمَّا
ظَلَمُواْ
وَجَآءَتۡهُمۡ
رُسُلُهُم
بِٱلۡبَيِّنَٰتِ
وَمَا
كَانُواْ
لِيُؤۡمِنُواْۚ
كَذَٰلِكَ
نَجۡزِي
ٱلۡقَوۡمَ
ٱلۡمُجۡرِمِينَ
١٣
Na kwa yakini tumekwisha ziangamiza kaumu za kabla yenu walipo dhulumu, na waliwajia Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi; lakini hawakuwa wenye kuamini. Ndio kama hivyo tunavyo walipa watu wakosefu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika tuliwaangamiza watu waliowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu kabla yenu, enyi mliomshirikisha Mola wenu, waliposhirikisha na wakawajia Mitume wao kutoka kwa Mwenyezi Mungu wakiwa na miujiza iliyo wazi na hoja zenye kubainisha ukweli wa yale aliyekuja nayo. Basi watu hawa hawakuwa ni wenye kuwaamini Mitume wao na kuwafuata, kwa hivyo walistahili maangamivu. Na mfano wa maangamivu hayo ndivyo atakavyolipwa kila mhalifu mwenyekukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu.