Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:28

10:28
ويوم نحشرهم جميعا ثم نقول للذين اشركوا مكانكم انتم وشركاوكم فزيلنا بينهم وقال شركاوهم ما كنتم ايانا تعبدون ٢٨
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًۭا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَآؤُكُمْ ۚ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَآؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ ٢٨
وَيَوۡمَ
نَحۡشُرُهُمۡ
جَمِيعٗا
ثُمَّ
نَقُولُ
لِلَّذِينَ
أَشۡرَكُواْ
مَكَانَكُمۡ
أَنتُمۡ
وَشُرَكَآؤُكُمۡۚ
فَزَيَّلۡنَا
بَيۡنَهُمۡۖ
وَقَالَ
شُرَكَآؤُهُم
مَّا
كُنتُمۡ
إِيَّانَا
تَعۡبُدُونَ
٢٨
Na siku tutakapo wakusanya wote, kisha tutawaambia walio shirikisha:Simameni mahali penu nyinyi na wale mlio wafanya washirika. Kisha tutawatenga baina yao. Na hao walio washirikisha watasema: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kumbuka, ewe Mtume, Siku ambayo tutawafufua viumbe wote ili wahesabiwe na walipwe, kisha tuseme kuwaambia waliomshirikisha Mwenyezi Mungu, «Jilazimisheni mahali mliopo, nyinyi na washirika wenu ambao mlikuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, mpaka tuangalie mtafanya nini.» Hapo tutapambanua baina ya washirikina na wale wanaowaabudu, na watajitenga, wale walioabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, na wale waliokuwa wanawaabudu, na watasema kuwaambia washirikina «Hamkuwa mkituabudu sisi ulimwenguni.»