Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:35

10:35
قل هل من شركايكم من يهدي الى الحق قل الله يهدي للحق افمن يهدي الى الحق احق ان يتبع امن لا يهدي الا ان يهدى فما لكم كيف تحكمون ٣٥
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَهْدِىٓ إِلَى ٱلْحَقِّ ۚ قُلِ ٱللَّهُ يَهْدِى لِلْحَقِّ ۗ أَفَمَن يَهْدِىٓ إِلَى ٱلْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّىٓ إِلَّآ أَن يُهْدَىٰ ۖ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ٣٥
قُلۡ
هَلۡ
مِن
شُرَكَآئِكُم
مَّن
يَهۡدِيٓ
إِلَى
ٱلۡحَقِّۚ
قُلِ
ٱللَّهُ
يَهۡدِي
لِلۡحَقِّۗ
أَفَمَن
يَهۡدِيٓ
إِلَى
ٱلۡحَقِّ
أَحَقُّ
أَن
يُتَّبَعَ
أَمَّن
لَّا
يَهِدِّيٓ
إِلَّآ
أَن
يُهۡدَىٰۖ
فَمَا
لَكُمۡ
كَيۡفَ
تَحۡكُمُونَ
٣٥
Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina anaye ongoa kwendea Haki? Sema: Mwenyezi Mungu anaongoa kwendea Haki. Basi, je, anaye stahiki kufuatwa ni yule Mwenye kuongoa kwendea Haki au asiye ongoa ila aongozwe yeye? Basi nyinyi mna nini? Mnahukumu namna gani? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Je, kuna yoyote, miongoni mwa washirika wenu, mwenye kuongoza kwenye njia iliyolingana sawa?» Hakika wao hawawezi hilo. Waambie, «Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anamuongoza aliyepotea njia ya uongofu na kumuelekeza kwenye haki. Basi ni yupi anayefaa zaidi kufuatwa: ni yule anayeongoza, peke yake, kwenye njia ya haki au ni yule ambaye haongoki, kwa kutojua kwake na kwa upotevu wake, nao ndio hao washirikina wenu ambao hawaongozi wala hawaongoki mpaka waongozwe? Basi muna nini nyinyi, vipi mnamsawazisha Mwenyezi Mungu na viumbe vyake?» Huu ni uamuzi uliotanguka.