Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:39

10:39
بل كذبوا بما لم يحيطوا بعلمه ولما ياتهم تاويله كذالك كذب الذين من قبلهم فانظر كيف كان عاقبة الظالمين ٣٩
بَلْ كَذَّبُوا۟ بِمَا لَمْ يُحِيطُوا۟ بِعِلْمِهِۦ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُۥ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلظَّـٰلِمِينَ ٣٩
بَلۡ
كَذَّبُواْ
بِمَا
لَمۡ
يُحِيطُواْ
بِعِلۡمِهِۦ
وَلَمَّا
يَأۡتِهِمۡ
تَأۡوِيلُهُۥۚ
كَذَٰلِكَ
كَذَّبَ
ٱلَّذِينَ
مِن
قَبۡلِهِمۡۖ
فَٱنظُرۡ
كَيۡفَ
كَانَ
عَٰقِبَةُ
ٱلظَّٰلِمِينَ
٣٩
Bali wameyakanusha wasio yaelewa ilimu yake kabla hayajawajia maelezo yake. Kadhaalika walio kabla yao walikanusha vile vile. Basi angalia jinsi ulivyo kuwa mwisho wa madhaalimu hao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Bali wao walifanya haraka kuikanusha Qur’ani mwanzo walipoisikia, kabla hawajazizingatia aya zake, na wakakikanusha kitu ambacho wao hawana ujuzi nacho, miongoni mwa habari ya Ufufuzi, Malipo, Pepo, Moto na vinginevyo, na bado haujawajia wao uhakika wa yale waliyoahidiwa katika Kitabu. Na kama walivyokanusha washirikina mambo Aliyowaonya nayo Mwenyezi Mungu, ndivyo walivyokanusha watu waliopita kabla yao. Basi tazama, ewe Mtume, ulikuwaje mwisho wa madhalimu? Baadhi yao Mwenyezi Mungu Aliwaangamiza kwa kuwadidimiza ardhini, wengine kwa kuwazamisha majini na wengine kwa kuwapa mateso mengineyo.