Na wakikukanusha wewe, sema: Mimi nina a'mali yangu, na nyinyi mna a'mali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa niyatendayo, wala mimi sina jukumu kwa myatendayo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wakikukanusha, ewe Mtume, washirikina hawa waambie, «Mimi nina Dini yangu na matendo yangu, na nyinyi muna dini yenu na matendo yenu; nyinyi hamtaadhibiwa kwa matendo yangu, na mimi sitaadhibiwa kwa matendo yenu.»