Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:65

10:65
ولا يحزنك قولهم ان العزة لله جميعا هو السميع العليم ٦٥
وَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّ ٱلْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا ۚ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ ٦٥
وَلَا
يَحۡزُنكَ
قَوۡلُهُمۡۘ
إِنَّ
ٱلۡعِزَّةَ
لِلَّهِ
جَمِيعًاۚ
هُوَ
ٱلسَّمِيعُ
ٱلۡعَلِيمُ
٦٥
Wala yasikuhuzunishe maneno yao. Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na yasikusikitishe, ewe Mtume, maneno ya washirikina juu ya Mola wao na kumzulia kwao Yeye urongo na kuishirikisha kwao mizimu ya masanamu pamoja na Yeye. Kwani Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyepwekeka kwa nguvu zilizokamilika na uwezo uliotimia, ulimwenguni na Akhera; na Yeye Ndiye Msikizi wa maneno yao Ndiye Mjuzi wa nia zao na matendo yao.