Walipo tupa, Musa alisema: Mliyo leta ni uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu haitengenezi kazi ya waharibifu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Walipozitupa kamba zao na fimbo zao, Mūsā aliwaambia, «Mlivyokuja navyo mkavitupa ni uchawi. Mwenyezi Mungu Ataviondoa mlivyokuja navyo na atavitangua. Hakika Mwenyezi Mungu Hakitengenezi kitendo cha anayetembea katika ardhi ya Mwenyezi Mungu kufanya mambo Anayoyachukia na kufanya uharibifu humo kwa kumuasi.