Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Waambie, ewe Mtume, «Hii ni njia yangu, ninaita kwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, nikiwa kwenye hoja inayotoka kwa Mwenyezi Mungu na uhakika, mimi na anayenifuata. Na ninamuepusha Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, na washirika na mimi si katika wale wanaomshirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu mtu mwingine.»