Yusuf akasema: Yeye ndiye aliye nitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliye kuwa katika jamaa za mwanamke alisema: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Yūsuf akasema, «Yeye ndiye aliyetaka hilo kwangu. Na akatoa ushahidi mtoto wa mlezini katika jamaa zake(mke wa kiongozi) na akasema, «Iwapo kanzu yake imepasuka kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli katika tuhma alizomfanyia na yeye (Yūsuf) ni miongoni mwa warongo.