(Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ya’qūb, amani imshukiye, alisema kumwambia mwanawe Yūsuf, «Ewe Mwanangu, usiwatajie ndugu zako ndoto hii, watakuhusudu, watakufanyia uadui na watafanya hila za kukuua, hakika Shetani kwa binadamu ni adui ambaye uadui wake uko waziwazi.