Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi mbali ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi. Na baada ya haya mtakuwa watu wema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
«Muueni Yūsuf! Au mtupeni kwenye ardhi isiyojulikana iliyo mbali na mji, hapo yatasafika kwenu mapenzi ya baba yenu na muelekeo wake kwenu, na hatageuka kwa wengine na kuacha kushughulika na nyinyi, na mtakuwa, baada ya kumuua Yūsuf au kumuepusha, ni wenye kutubia kwa Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha baada ya kosa lenu.»