Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:103

3:103
واعتصموا بحبل الله جميعا ولا تفرقوا واذكروا نعمت الله عليكم اذ كنتم اعداء فالف بين قلوبكم فاصبحتم بنعمته اخوانا وكنتم على شفا حفرة من النار فانقذكم منها كذالك يبين الله لكم اياته لعلكم تهتدون ١٠٣
وَٱعْتَصِمُوا۟ بِحَبْلِ ٱللَّهِ جَمِيعًۭا وَلَا تَفَرَّقُوا۟ ۚ وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَآءًۭ فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِۦٓ إِخْوَٰنًۭا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍۢ مِّنَ ٱلنَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ١٠٣
وَٱعۡتَصِمُواْ
بِحَبۡلِ
ٱللَّهِ
جَمِيعٗا
وَلَا
تَفَرَّقُواْۚ
وَٱذۡكُرُواْ
نِعۡمَتَ
ٱللَّهِ
عَلَيۡكُمۡ
إِذۡ
كُنتُمۡ
أَعۡدَآءٗ
فَأَلَّفَ
بَيۡنَ
قُلُوبِكُمۡ
فَأَصۡبَحۡتُم
بِنِعۡمَتِهِۦٓ
إِخۡوَٰنٗا
وَكُنتُمۡ
عَلَىٰ
شَفَا
حُفۡرَةٖ
مِّنَ
ٱلنَّارِ
فَأَنقَذَكُم
مِّنۡهَاۗ
كَذَٰلِكَ
يُبَيِّنُ
ٱللَّهُ
لَكُمۡ
ءَايَٰتِهِۦ
لَعَلَّكُمۡ
تَهۡتَدُونَ
١٠٣
Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Shikamaneni nyote na Kitabu cha Mola wenu na uongofu wa Mtume wenu, wala msitende ambayo yatapelekea kutengana kwenu. Na ikumbukeni neema kubwa ambayo Mwenyezi Mungu Amewaneemesha nayo, pindi mlipokuwa, enyi Waumini, kabla ya Uislamu ni maadui, Mwenyezi Mungu Akazikusanya nyoyo zenu juu ya kumpenda Yeye na kumpenda Mtume Wake, na akatia ndani ya nyoyo zenu mahaba ya kupendana wenyewe kwa wenyewe, hapo mkawa, kwa fadhila Zake, ni ndugu mpedanao. Na mlikuwa kwenye ukingo wa moto wa Jahanamu, Mwenyezi Mungu Akawaongoza kwa Uislamu na Akawaokoa na Moto. Na kama Mwenyezi Mungu Alivyowafunulia wazi alama za imani iliyo sahihi, hivyo hivyo Anawabainishia yote yale ambayo ndani yake muna kutengenea kwenu, mpate kuongoka kweye njia ya uongofu na mpate kuiandama ili msipotee mkaiepuka.