Na pale ulipo toka asubuhi, ukaacha ahali zako uwapange Waumini kwenye vituo kwa ajili ya vita - na Mwenyezi Mungu anasikia na anajua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kumbuka,ewe Mtume, pindi ulipotoka nyumbani kwako, ukiwa umevaa mavazi ya vita, huku wazipanga safu za Masahaba wako, na unamuweka kila mmoja mahali pake ili kukutana na washirikina katika vita vya Uhud. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzisikia kauli zenu, ni Mwenye kuvijua vitendo vyenu.