Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hao waliosifiwa kwa sifa hizo, malipo yao ni kwamba Mwenyezi Mungu Atayasitiri madhambi yao na watapata mabustani ya Peponi ambayo maji tamu yatakuwa yanapita chini ya miti yake na majumba yake ya fahari, ilhali ya kukaa humo milele; hawatotoka humo kamwe. Na malipo bora ya wenye kutenda mema ni msamaha na Pepo.