Ambao husema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na tuepushe na adhabu ya Moto, 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Waja hawa wacha-Mungu huwa wakisema, «Mola wetu, sisi tumekuamini Wewe na tumemfuata Mtume Wako Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, tusamehe madhambi tuliyoyatenda na utuepushe na adhabu ya Moto.»