Je! Aliye yafuata ya kumridhisha Mwenyezi Mungi ni kama yule aliye stahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yake yakawa Jahannamu? Napo ni mahala pabaya pa kurejea. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Yule ambaye lengo lake ni radhi za Mwenyezi Mungu, halingani na yule ambaye ametopea kwenye maasia na kumkasirisha Mola wake na akastahiki kwa hilo makazi ya Jahanamu ambayo mwisho mbaya wa mtu kuishilia ni hapo.