Basi itakuwaje tutakapo wakusanya Siku ambayo haina shaka kuja kwake? Na kila nafsi italipwa kama ilivyo chuma, bila ya kudhulumiwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Vipi hali zao zitakuwa, Atakapowakusanya Mwenyezi Mungu ili wahesabiwe katika Siku isiyo na shaka kuja kwake, nayo ni Siku ya Kiyama, na kila mmoja apate malipo ya aliyoyatenda, na wao bila kudhulumiwa kitu chochote?