Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:30

3:30
يوم تجد كل نفس ما عملت من خير محضرا وما عملت من سوء تود لو ان بينها وبينه امدا بعيدا ويحذركم الله نفسه والله رءوف بالعباد ٣٠
يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍۢ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍۢ مُّحْضَرًۭا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوٓءٍۢ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُۥٓ أَمَدًۢا بَعِيدًۭا ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفْسَهُۥ ۗ وَٱللَّهُ رَءُوفٌۢ بِٱلْعِبَادِ ٣٠
يَوۡمَ
تَجِدُ
كُلُّ
نَفۡسٖ
مَّا
عَمِلَتۡ
مِنۡ
خَيۡرٖ
مُّحۡضَرٗا
وَمَا
عَمِلَتۡ
مِن
سُوٓءٖ
تَوَدُّ
لَوۡ
أَنَّ
بَيۡنَهَا
وَبَيۡنَهُۥٓ
أَمَدَۢا
بَعِيدٗاۗ
وَيُحَذِّرُكُمُ
ٱللَّهُ
نَفۡسَهُۥۗ
وَٱللَّهُ
رَءُوفُۢ
بِٱلۡعِبَادِ
٣٠
Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iliyo yafanya yamehudhurishwa, na pia ubaya ilio ufanya. Itapenda nafsi lau kungekuwako masafa marefu baina ya ubaya huo na yeye. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na katika Siku ya Kiyama, Siku ya Malipo, kila nafsi italikuta jema lolote ililolifanya linaingojea likiwa limeongezwa ili ilipwe nalo. Na pia baya iliolifanya italikuta linaingojea vilevile, hapo itatamani lau ilikuwa baina yake na hilo tendo baya zama zirefu. Basi jitayarisheni kwa Siku hii, na muogope mateso ya Mola Aliye Jabari. Na pamoja na ukali wa mateso Yake, Yeye, Aliyetakata na sifa za upungufu, ni Msifika kwa ukamilifu wa huruma kwa waja.