Akasema Zakariya: Mola wangu Mlezi! Vipi nitapata mwana na hali ukongwe umenifikia, na mke wangu ni tasa? Akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Zakariyyā akasema akiwa na furaha na kwa kustaajabu, «Mola wangu! Vipi nitakuwa na mtoto hali ya kuwa uzee umenifikia hadi ya kunifikia na mke wangu ni tasa, hazai.? Akasema, «Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu Anavyofanya Anayoyataka katika mambo ya ajabu yanayokwenda kinyume na mambo ya kawaida.»