Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:50

3:50
ومصدقا لما بين يدي من التوراة ولاحل لكم بعض الذي حرم عليكم وجيتكم باية من ربكم فاتقوا الله واطيعون ٥٠
وَمُصَدِّقًۭا لِّمَا بَيْنَ يَدَىَّ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ ٱلَّذِى حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚ وَجِئْتُكُم بِـَٔايَةٍۢ مِّن رَّبِّكُمْ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ٥٠
وَمُصَدِّقٗا
لِّمَا
بَيۡنَ
يَدَيَّ
مِنَ
ٱلتَّوۡرَىٰةِ
وَلِأُحِلَّ
لَكُم
بَعۡضَ
ٱلَّذِي
حُرِّمَ
عَلَيۡكُمۡۚ
وَجِئۡتُكُم
بِـَٔايَةٖ
مِّن
رَّبِّكُمۡ
فَٱتَّقُواْ
ٱللَّهَ
وَأَطِيعُونِ
٥٠
Na ninasadikisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale mlio harimishiwa, na nimekujieni na Ishara kutokana na Mola Mlezi wenu. Kwa hivyo mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
«Na nimewajia nyinyi kuyasadikisha yaliyomo ndani ya Taurati, na ili niawahalalishie, kwa wahyi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu, baadhi ya yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaharamishia, yakiwa ni usahilishaji na huruma kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na nimewajia na hoja kutoka kwa Mola wenu ya ukweli wa ninayowaambia. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu na msiende kinyume na amri Yake na mnitii mimi katika yale ninayowafikishia kutoka kwa Mwenyezi Mungu.