Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu ilhali nyinyi mnashuhudia? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi watu wa Taurati na Injili! Vipi nyinyi mnakanusha aya za Mwenyezi Mungu ambazo aliziteremsha kwa Mitume wake katika Vitabu vyenu, na ndani yake muna kuwa Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ndiye Mtume anayengojewa na kuwa aliyowajia nayo ndio haki. Na nyinyi mnashuhudia hilo, lakini mnalikanusha.