Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Je, hawa washirikina ni bora au watu wa Tubba’ wa Himyar na wale waliokuwa kabla yao miongoni mwa ummah waliomkanusha Mola wao? Tuliwaangamiza kwa uhalifu wao na kukanusha kwao. Hawa washirikina si bora kuliko hao ili tuwasamehe na tusiwaangamize, na hali wao wanamkanusha Mwenyezi Mungu.