Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:123

7:123
قال فرعون امنتم به قبل ان اذن لكم ان هاذا لمكر مكرتموه في المدينة لتخرجوا منها اهلها فسوف تعلمون ١٢٣
قَالَ فِرْعَوْنُ ءَامَنتُم بِهِۦ قَبْلَ أَنْ ءَاذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَمَكْرٌۭ مَّكَرْتُمُوهُ فِى ٱلْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا۟ مِنْهَآ أَهْلَهَا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ١٢٣
قَالَ
فِرۡعَوۡنُ
ءَامَنتُم
بِهِۦ
قَبۡلَ
أَنۡ
ءَاذَنَ
لَكُمۡۖ
إِنَّ
هَٰذَا
لَمَكۡرٞ
مَّكَرۡتُمُوهُ
فِي
ٱلۡمَدِينَةِ
لِتُخۡرِجُواْ
مِنۡهَآ
أَهۡلَهَاۖ
فَسَوۡفَ
تَعۡلَمُونَ
١٢٣
Akasema Firauni: Mmemuamini kabla sijakupeni idhini? Hizi ni njama mlizo panga mjini mpate kuwatoa wenyewe. Lakini karibu mtajua! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Fir'awn akasema kuwaambia wachawi, «Mumemuamini Mwenyezi Mungu kabla sijawapa idhini mumuamini? Hakika kumuamini kwenu Mwenyezi Mungu, kumsadiki kwenu Mūsā na kuukubali kwenu unabii wake ni hila mlizozipanga nyinyi na Mūsā ili muwatoe watu wa mji wenu kutoka humo, na ili muzivamie heri zake na mufaidike nazo peke yenu.Basi mtajua, enyi wachawi, adhabu na mateso yatakayowashukia nyinyi.