Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Ahqaf 46:10

46:10
قل ارايتم ان كان من عند الله وكفرتم به وشهد شاهد من بني اسراييل على مثله فامن واستكبرتم ان الله لا يهدي القوم الظالمين ١٠
قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ وَكَفَرْتُم بِهِۦ وَشَهِدَ شَاهِدٌۭ مِّنۢ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ عَلَىٰ مِثْلِهِۦ فَـَٔامَنَ وَٱسْتَكْبَرْتُمْ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ١٠
قُلۡ
أَرَءَيۡتُمۡ
إِن
كَانَ
مِنۡ
عِندِ
ٱللَّهِ
وَكَفَرۡتُم
بِهِۦ
وَشَهِدَ
شَاهِدٞ
مِّنۢ
بَنِيٓ
إِسۡرَٰٓءِيلَ
عَلَىٰ
مِثۡلِهِۦ
فَـَٔامَنَ
وَٱسۡتَكۡبَرۡتُمۡۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
لَا
يَهۡدِي
ٱلۡقَوۡمَ
ٱلظَّٰلِمِينَ
١٠
Sema: Mwaonaje yakiwa haya ni kweli yametoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi mmeyakataa, na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini, na nyinyi mnafanya kiburi? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema , ewe Mtume, uwaambie washirikina wa watu wako, “Nipasheni habari: ikiwa hii Qur’ani inatoka kwa Mwenyezi Mungu na mkaikanusha, na hali ameshuhudia shahidi kati ya Wana wa Isrāīl, kama ‘Abdullāh bin Salām, kwa mfano wa hii Qur’ani, nayo ni yaliyomo ndani ya Taurati ya kusadikisha unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, akaiamini na akayafuata kivitendo yaliyokuja ndani ya Qur’ani, na nyinyi mkakanusha hilo kwa njia ya kiburi. Basi ni upi huu isipokuwa ni udhalimu mkubwa na ukafiri mwingi?” Hakika Mwenyezi Mungu Hawaongozi kwenye Uislamu na kuifikia haki wale watu waliojidhulumu kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu.