Basi walipo liona wingu likielekea kwenye mabonde yao, walisema: Wingu hili la kutunyeshea mvua! Kumbe sivyo, haya ni hayo mliyo yahimiza, upepo ambao ndani yake imo adhabu chungu! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Walipoiona adhabu walioifanyia haraka imejitokeza juu ikielekea kwenye mabonde yao, walisema, “Hiki ni kiwingu chenye kutunyesheza mvua.” Hūd, amani imshukie, aliwaambia, «Hiki si kiwingu cha mvua na rehema kama mlivyodhania, bali hiki ni kiwingu cha adhabu mliyoitaka kwa haraka, huo ni upepo ambao ndani yake muna adhabu yenye uchungu na yenye kuumiza.