Unaangamiza kila kitu kwa amri ya Mola wake Mlezi. Wakawa hawaonekani ila nyumba zao tu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wakosefu! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
«Unaangamiza kila kitu unachokipitia katika vitu ambavyo ulitumwa uviangamize kwa amri ya Mola wake na matakwa Yake.» Wakawa hakuna kinachoonekana chochote katika miji yao isipokuwa nyumba zao walizokuwa wakizikaa. Mfano wa malipo haya ndiyo tunayowalipa makafiri kwa sababu ya uhalifu wao na kupita kiasi kwao.