NA MIONGONI mwenu atakeye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki ya ukarimu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kati yenu na akafanya matendo Aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu , tutampa malipo mema ya matendo yake mara mbili zaidi ya malipo ya asiyekuwa yeye kati ya wanawake wengine, na tumemuandalia yeye riziki nzuri, nayo ni Pepo.