Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika ya wale wanaomuudhi Mwenyezi Mungu kwa kumshirikisha na kufanya maasia mengine, na wakamuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa maneno na vitendo, Mwenyezi Mungu atawafukuza na Atawaweka mbali na kheri duniani na Akhera, na Amewaandalia, huko Akhera, adhabu kali yenye kuwadhalilisha na kuwafanya wanyonge.