Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na jihadharini, enyi Waumini, na mtihani na mkasa yenye kuwaenea waliofanya makosa na wasiofanya, hawahusishwi nayo wenye maasia wala aliyefanya dhambi; bali yanawapata watu wema pamoja nao iwapo wanaweza kukataza udhalimu wasiukataze. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa mateso kwa mwenye kwenda kinyume na maamrisho Yake na makatazo Yake.