Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema alizo waneemesha watu, mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao. Na hakika Mwwnyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Malipo hayo maovu ni kwamba Mwenyezi Mungu pindi Anapowaneemesha watu neema yoyote, hawaondolei mpaka wabadilishe hali yao njema iwe mbovu, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzijua hali zao, kwa hivyo huwapitishia yale yaliyolingana na ujuzi Wake na matakwa Yake.