Basi kuleni katika mlivyo teka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Basi kuleni mlichokipata katika ngawira na fidia ya mateka, kwani hiyo ni halali nzuri. Na jilazimisheni na hukumu za Mwenyezi Mungu na sheria Zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwenye huruma nao.