Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
2:102
واتبعوا ما تتلو الشياطين على ملك سليمان وما كفر سليمان ولاكن الشياطين كفروا يعلمون الناس السحر وما انزل على الملكين ببابل هاروت وماروت وما يعلمان من احد حتى يقولا انما نحن فتنة فلا تكفر فيتعلمون منهما ما يفرقون به بين المرء وزوجه وما هم بضارين به من احد الا باذن الله ويتعلمون ما يضرهم ولا ينفعهم ولقد علموا لمن اشتراه ما له في الاخرة من خلاق ولبيس ما شروا به انفسهم لو كانوا يعلمون ١٠٢
وَٱتَّبَعُوا۟ مَا تَتْلُوا۟ ٱلشَّيَـٰطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَـٰنَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَـٰنُ وَلَـٰكِنَّ ٱلشَّيَـٰطِينَ كَفَرُوا۟ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحْرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَـٰرُوتَ وَمَـٰرُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌۭ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيْنَ ٱلْمَرْءِ وَزَوْجِهِۦ ۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا۟ لَمَنِ ٱشْتَرَىٰهُ مَا لَهُۥ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ مِنْ خَلَـٰقٍۢ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا۟ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ ١٠٢
وَٱتَّبَعُواْ
مَا
تَتۡلُواْ
ٱلشَّيَٰطِينُ
عَلَىٰ
مُلۡكِ
سُلَيۡمَٰنَۖ
وَمَا
كَفَرَ
سُلَيۡمَٰنُ
وَلَٰكِنَّ
ٱلشَّيَٰطِينَ
كَفَرُواْ
يُعَلِّمُونَ
ٱلنَّاسَ
ٱلسِّحۡرَ
وَمَآ
أُنزِلَ
عَلَى
ٱلۡمَلَكَيۡنِ
بِبَابِلَ
هَٰرُوتَ
وَمَٰرُوتَۚ
وَمَا
يُعَلِّمَانِ
مِنۡ
أَحَدٍ
حَتَّىٰ
يَقُولَآ
إِنَّمَا
نَحۡنُ
فِتۡنَةٞ
فَلَا
تَكۡفُرۡۖ
فَيَتَعَلَّمُونَ
مِنۡهُمَا
مَا
يُفَرِّقُونَ
بِهِۦ
بَيۡنَ
ٱلۡمَرۡءِ
وَزَوۡجِهِۦۚ
وَمَا
هُم
بِضَآرِّينَ
بِهِۦ
مِنۡ
أَحَدٍ
إِلَّا
بِإِذۡنِ
ٱللَّهِۚ
وَيَتَعَلَّمُونَ
مَا
يَضُرُّهُمۡ
وَلَا
يَنفَعُهُمۡۚ
وَلَقَدۡ
عَلِمُواْ
لَمَنِ
ٱشۡتَرَىٰهُ
مَا
لَهُۥ
فِي
ٱلۡأٓخِرَةِ
مِنۡ
خَلَٰقٖۚ
وَلَبِئۡسَ
مَا
شَرَوۡاْ
بِهِۦٓ
أَنفُسَهُمۡۚ
لَوۡ
كَانُواْ
يَعۡلَمُونَ
١٠٢
Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na Mayahudi walifuata yale ambayo mashetani walikuwa wanawasimulia wachawi katika kipindi cha ufalme wa Sulaimān mwana wa Dāwūd. Na Sulaymān hakukufuru na wala hakujifundisha uchawi. Lakini mashetani ndio walimkanusha Mwenyezi Mungu kwa kuwafundisha watu uchawi, kwa kuwaharibia dini yao. Mayahudi pia waliufuata uchawi ulioshushwa kwa malaika wawili: Hārūt na Mārūt, katika ardhi ya Babil ilyoko Iraq, ukiwa ni mtihani na majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja Wake. Na hao Malaika wawili hawakuwa wakimfunza yoyote mpaka wamnasihi na kumuonya asijifunze uchawi na kumwambia, “Usikufuru kwa kujifunza uchawi na kuwatii mashetani.” Basi watu walikuwa wakijifunza kutoka kwa Malaika wawili vitu vinavyozusha chuki baina ya mume na mke mpaka wakafarikana. Na wachawi hawana uwezo wa kumdhuru, kwa uchawi wao, yoyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na hukumu Yake. Na wachawi hawajifunzi ila shari yenye kuwadhuru na kutowapa nafuu. Mashetani waliupeleka uchawi kwa Mayahudi, ukaenea kwao mpaka wakaufadhilisha juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Na Mayahudi walijua kwamba mwenye kuchagua uchawi na kuacha haki, hatakuwa na fungu lolote la kheri huko Akhera. Ni ubaya ulioje uchawi na ukafiri waliojichagulia nafsi zao kuwa ni badala ya Imani na kumfuata Mtume, lau walikuwa na elimu yenye kuzalisha vitendo vya kufuata mawaidha wapewayo!