Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Jilazimisheni na Dini ya Mwenyezi Mungu ambayo Ameifanya inasibiane na maumbile yenu. Kwani hakuna maumbile mazuri kuliko yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewaumbia watu. Jilazimisheni nayo na mseme, “Sisi ni wenye kuiandama, ni watiifu kwa Mola wetu katika kufuata kwetu mila ya Ibrāhīm.”