Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na baadhi ya watu huziuza nafsi zao kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, kwa kupigana jihadi katika njia Yake na kujilazimisha kumtii. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja, Anawarehemu waja wake Waumini rehema kunjufu, katika ulimwengu wao na Akhera yao, na kuwalipa malipo mazuri zaidi.