Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola na Muhammad kuwa ndiye Mtume na Uislamu kuwa ndiyo Dini, ingieni katika sheria zote za Uislamu, hali ya kutekeleza hukumu zake zote, wala msiache chochote kati yazo, wala msiandame njia za Shetani katika yale anayowaitia ya maasia.Hakika Shetani kwenu ni adui mwenye uadui uliyo wazi. Basi jihadharini naye.