Mwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi. Bali anakushikeni kwa yanayo chuma nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Mwenyezi Mungu Hatawaadhibu nyinyi kwa sababu ya viyapo vyenu mnavyoviapa bila kukusudia, lakini Atawaadhibu kwa viapo vilivyokusudiwa na nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe kwa yule anayetubia Kwake, ni Mpole kwa mwenye kumuasi kwa kuwa hamharakishii mateso.