Zilindeni Swala, na khasa Swala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea). 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Zihifadhini, enyi Waislamu, Swala tano zilizofaradhiwa kwa kudumu nazo katika kuzitekeleza kwa nyakati zake, masharuti yake, nguzo zake yanayopasa yake. Na muhufadhi swala iliyo katikati ya swala hizo, nayo ni Swala ya Alasir Na simameni katika Swala zenu hali ya kumtii Mwenyezi Mungu, kumnyenyekea na kumdhalilikia.