Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayo fuatiliwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha na Mpole. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Maneno mazuri kujibiwa muombaji na kusamehe utiriri wake katika kuomba, ni bora kuliko sadaka inayofuatiwa na kero na ubaya kutoka kwa mtoaji sadaka. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Hana haja ya sadaka za waja, ni Mpole Hana haraka nao ya kuwatesa.