Al-Baqarah 2:268 الشيطان يعدكم الفقر ويامركم بالفحشاء والله يعدكم مغفرة منه وفضلا والله واسع عليم ٢٦٨
ٱلشَّيۡطَٰنُ
يَعِدُكُمُ
ٱلۡفَقۡرَ
وَيَأۡمُرُكُم
بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ
وَٱللَّهُ
يَعِدُكُم
مَّغۡفِرَةٗ
مِّنۡهُ
وَفَضۡلٗاۗ
وَٱللَّهُ
وَٰسِعٌ
عَلِيمٞ
٢٦٨
Shet'ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua. 1
Soma Tafsir
Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis
Uchoyo huu na kuchagua kibaya kukitoa sadaka yatokana na Shetani ambaye anawaogopesha nyinyi ufukara na kuwahimiza uchoyo, na anawaamrisha nyiyi maasia na kumfanyia kinyume Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kutukuka, Anawaahidi nyinyi, kwa kutoa kwenu, msamaha wa madhambi…
Uchoyo huu na kuchagua kibaya kukitoa sadaka yatokana na Shetani ambaye anawaogopesha nyinyi ufukara na kuwahimiza uchoyo, na anawaamrisha nyiyi maasi…