Na chochote mnacho toa au nadhiri mnazo weka basi hakika Mwenyezi Mungu anajua. Na walio dhulumu hawana wa kuwanusuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mali yoyote mnayoyatoa na mengineyo, machache au mengi, au sadaka mnayoitoa kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, au mkajilazimisha nafsi zenu chochote, cha mali au kinginecho, basi Mwenyezi Mungu Anayajua hayo; na Yeye Ndiye Mwenye kuchungulia nia zenu, na Atawalipa kwa hayo. Na yoyote mwenye kuzuia haki ya Mwenyezi Mungu ni dhalimu. Na madhalimu hawana wenye kuwanusuru ambao watawazuia wasipate adhabu ya Mwenyezi Mungu.