Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na ili kubainisha utukufu wa Ādam, Amani imshukiye, Mwenyezi Mungu Alimfundisha majina ya vitu vyote, kisha Akaviorodhesha hivyo vitu kwa Malaika na kuwaambia, “Niambieni majina ya vitu hivi vilivyoko, ikiwa nyinyi ni wakweli kwamba nyinyi mnastahiki zaidi uimarishaji wa ardhi kuliko wao.”